Manchester United Wameingia Sokoni Kwa Mwembwe

Kocha wa zamani wa Bayern Munich wa Chelsea Thomas Tuchel ni miongoni mwa orodha ya Manchester United ya watu wanaoweza kuchukua nafasi ya Erik ten Hag iwapo Mholanzi huyo ataondoka msimu wa joto. Hata hivyo Tuchel amefungua milango ya kusalia Bayern Munich baada ya msimu huu licha ya kutangazwa Februari kwamba ataondoka.

Manchester United imefanya mawasiliano na wakala wa kiungo wa kati wa kimataifa wa Ufaransa Adrien Rabiot, 29, ambaye mkataba wake na Juventus unakamilika msimu huu wa joto.

Everton wanatumani ya kumshawishi Jarrad Branthwaite, 21, kusalia Goodison Park kwa mwaka mmoja zaidi lakini Manchester United wana imani kwamba dau la £60-70m kwa beki huyo wa kati wa Uingereza litakubaliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *