Man Utd Wapata Pigo Jingine kwa Jeraha la Beki Harry Maguire.

Harry Maguire

Klabu ya Manchester United imetangaza kwamba beki wake Harry Maguire atakuwa nje ya uwanja kwa muda wote uliobaki wa msimu huu kutokana na jeraha la msuli. Muingereza huyo, ambaye amekuwa muhimu katika safu ya ulinzi ya United msimu huu, anatajwa kuwa anaangaziw akwa ukaribu ili kubaini iwapo ataweza kurejea kabla ya mwisho wa mwezi Mei.

Taarifa iliyotolewa na usimamizi wa Manchester United siku ya Jumapili imebainisha kwamba Maguire atahitaji muda wa majuma matatu kupata nafuu kabla ya kurejea uwanjani baada ya kupata jeraha wakati wa mazoezi. Ingawa maelezo zaidi kuhusu jeraha lake hayakutolewa, inaonekana kuwa ni jeraha lenye kumfanya ashindwe kucheza kwa muda wa wiki kadhaa.

Kutowepo kwa Maguire kwenye kikosi cha United kunazua wasiwasi kuhusu mechi zilizobaki za ligi, pamoja na fainali ya Kombe la FA dhidi ya mahasimu wao, Manchester City. Hata hivyo, kuna matumaini kwamba beki huyo wa kimataifa wa Uingereza atakuwa tayari kwa michuano ya EURO inayokuja mwezi Juni.

Jeraha la Maguire linakuja kama pigo lingine kwa meneja wa Manchester United, Erik ten Hag, ambaye amekuwa akilazimika kufanya mabadiliko kwenye kikosi chake kutokana na majeraha ya mara kwa mara ya wachezaji muhimu kama vile Luke Shaw, Lisandro Martinez, Raphael Varane, Casemiro, na Mason Mount.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *