City Stars Walazimisha sare ya 1-1 Dhidi ya Ulinzi Katika Mchuano wa Ligi.

City Stars Vs Ulinzi
Kilabu ya Nairobi City Stars imefanikiwa kutoka nyuma na kulazimisha sare ya 1-1 kwenye mpambano wa ligi kuu ya humu nchini ulioandaliwa mwendo wa saa sita mchana wa leo kwenye uwanja wa Dandora.
Wanajeshi wa Ulinzi walikuwa wa kwanza kucheka na nyavu za wenyeji wao kupitia mchezaji Boniface Muchiri katika dakika ya 22 na kuwahakikishia Ulinzi uongozi wa 1-0 kuelekea kwenye kipindi cha mapumziko. City Stars hata hivyo hawakua tayari kudondosha alama zote tatu na walipata kurejesha hali kuwa sawa kwa bao la dakika ya 71 ya mchezo kutoka kwa Vincent Owino.
Alama hiyo moja imewaskuma City stars alama moja mbele ya Bandari kwenye nafasi ya nne kwenye jedwali, huku wanajeshi wa ulinzi wakipiga hatua ya kuondolea hatari ya kushushwa ngazi wakiwa wanasalia katika nafasi ya 13 wakiwa na alama 31 baada ya kuingia uwanjani mara 28.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *