Miujiza ya Los Blancos: Real Madrid watinga Fainali ya UCL kwa Kuwaangusha Bayern.

Mabingwa mara 14 wa bara Ulaya Real Madrid, wamefuzu katika fainali ya Kombe la Klabu Bingwa Barani Ulaya mwaka huu baada ya kuishinda Bayern Munich kwa mabao 2-1 katika mchuano uliochezwa usiku wa jana katika Uwanja wa Santiago Bernabeu.

Mabao mawili ya dakika za mwisho kutoka kwa José Luis Mato Sanmartín, maarufu kama Joselu, yalisaidia Real Madrid kufikia ushindi huo, huku Bayern Munich wakipata bao moja lililofungwa na Alphonso Davies. Madrid walihifadhi nafasi yao kwa ushindi jumla wa mabao 4-3 baada ya mkondo wa kwanza ugani Allianz Arena kukamilika kwa sare ya 2-2.

Kufuatia ushindi huo, Real Madrid imejihakikishia nafasi yao katika fainali kwa mara ya 15, ambapo watapambana na Borussia Dortmund kwenye Uwanja wa Wembley tarehe mosi mwezi ujao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *