Shujaa Kupiga Kambi Miramas Kujiandaa kwa Mechi ya Kufuzu kwa HSBC

Shujaa

Kikosi cha Kenya cha mchezo wa raga kwa wachezaji saba kila upande, maarufu kama Shujaa, kitapiga kambi katika eneo la Miramas nchini Ufaransa, kujiandaa kwa awamu ya kufuzu kwa michuano ya HSBC World Series itakayofanyika mjini Madrid mwishoni mwa mwezi huu.

Vijana wa taifa, ambao walikamilisha mzunguko wa Munich katika nafasi ya tano, wanatumai wataweza kufuzu na kurejea kwenye mashindano ya HSBC. Pia, wanajinoa kwa ajili ya mashindano ya Olimpiki yatakayofanyika mwezi Julai mwaka huu huko Ufaransa.

Shujaa wamekuwa na mkondo mzuri katika michuano ya mizunguko ya kujitafutia nafasi ya kurejea kwenye mashindano ya HSBC, na wanatarajia kwamba kambi yao katika eneo la Miramas itawasaidia kujiimarisha kwa mashindano hayo muhimu.

Makundi yaliyoidhinishwa kwa ajili ya michuano ya Fainali ya kufuzu kwa HSBC huko Madrid.

Katika mchakato wa kujikatia tiketi ya kurudi kwenye mizunguko ya HSBC, vijana hao wa nyumbani watakabiliana na Spain, Samoa, na Chile kwenye Kundi B.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *