Harambee Stars Kumenyana na Cameroon, Namibia na Zimbabwe Kufuzu AFCON 2025

afcon

Timu ya taifa ya Harambee Stars imepangwa kucheza dhidi ya Cameroon, Namibia, na Zimbabwe katika kundi J la mechi za kufuzu kwa kipute cha AFCON 2025. Michuano hii ya kutafuta wahsiriki wa makala yajayo ya AFCON itaanza rasmi mwezi Septemba mwaka huu.

Baada ya Harambee Stars kukosa nafasi katika mechi za kufuzu zilizopita kutokana na marufuku ya shirikisho la usimamizi wa soka duniani FIFA, timu hiyo sasa inatarajia kutia fora na hata kurejea kwenye mashindano hayo ya bara la Afrika.

Kocha mkuu wa Harambee Stars, Engin Firat, ameeleza imani yake kuwa kikosi chake kina uwezo mkubwa wa kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika zitakazofanyika Desemba 2025 nchini Morocco. Akizungumza baada ya droo iliyofanyika Alhamisi 04.07.2024, Firat aliisisitiza uwezo wake wa kuiongoza Kenya kurejea katika mashindano hayo kwa mara ya kwanza tangu 2019.

Katika droo iliyoandaliwa hapo jana matokeo kwenye makundi yote 12 ni kama ifuatavyo.

AFCON 2025

SOMA PIA | Kenya Kuwafahamu Wapinzani Wake Katika Mechi za Kufuzu kwa AFCON 2025.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *