Kilabu ya Barcelona imemsimamisha kazi kocha wake Xavi Hernandez kutoka kwa wadhifa wake wa ukufunzi. Katika taarifa iliyochapishwa na usimamizi wa Barcelona siku ya Ijumaa, usimamizi wa Barca ukiongozwa na rais Joan Laporta, uliafikia uamuzi wa kumsimamisha kazi Xavi baada ya kikao kilichoandaliwa mapema leo.
Xavi mwenye umri wa miaka 44, alitangaza kwamba ataondoka Barcelona mwanzoni mwa mwaka huu, kabla yake kushawishiwa kubadili msimamo wake mwezi Aprili. Hata hivyo matamshi yake ya hivi majuzi kuhusu hali ya kifedha ya kilabu hiyo, imeonekana kuchemsha usimamizi wa Barca na kuchukua hatua ya kumtimua.
▶ FC Barcelona official statementhttps://t.co/yJRoC1n9YS
— FC Barcelona (@FCBarcelona) May 24, 2024
Taarifa hiyo ilieleza kwamba Xavi ataongoza kikosi cha Barcelona kwa mara ya mwisho katika mechi ijayo dhidi ya Sevilla. Barca aidha wanatarajiwa kumtangaza kocha mpya katika siku kadhaa zijazo, huku Hansi Flick akitajwa kama mmoja atakayetwaa nafasi ya kuwa mkufunzi mkuu wa Barcelona.