Chipukizi wa Kenya wa Soka ya U23 Waaga Mashindano ya COSAFA.

Timu ya taifa ya Chipukizi wa U23 (Emerging Stars), ilikubali kuyaaga mashindano ya mwaka huu ya COSAFA, baada ya kumaliza katika nafasi ya pili kwenye Kundi B wakiwa na alama sita, kufuatia kushinda mechi mbili na kupoteza mmoja kwenye awamu ya makundi.

Ushindi  wa mabao 3-1 ambao Angola na Namibia walivuna katika mechi zao dhidi ya Lesotho na Sychelles mtawalia hapo jana ulifunga nafasi ya Kenya, ambao walikuwa wanasubiri mmoja wa wawili hao kudondosha alama. Angola na Namibia waliomaliza katika nafasi ya kwanza na ya pili kwenye kundi C kwa alama saba kila moja, walitwaa nafasi mbili zilizokuwa zimebaki katika awamu ya nusu fainali na kuungana na Mozambique na Comoros.

Kenya walimaliza katika nafasi ya pili kwenye mashindano ya mwaka huu ambayo walishiriki kama wageni. Vijana wa taifa walianza kwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Zambia, kabla ya kupoteza kwa mabao sawia dhidi ya Comoros kwenye mchuano wa pili. Mchuano wa mwisho ulishuhudia vijana wa taifa wakifaidi na ushindi wa 2-0 dhidi ya Zimbabwe na kutinga alama 6 katika mechi 3.

GOR MAHIA WAPONA KWA KENYA KUONDOKA COSAFA

Matokeo haya, hata hivyo, yamekuwa afueni kwa kilabu ya Gor Mahia ambayo ilikuwa na idadi kubwa ya wachezaji katika kikosi cha Emerging Stars. Gor Mahia iliwakilishwa na wachezaji 6, ambao sasa watapata fursa ya kuungana na wenzao kwa ajili ya mashindano ya CECAFA Kagame Cup yanayotarajiwa kuanza Jumanne ijayo, tarehe 9 Julai 2024.

Gor Mahia Kumenyana na Al Hilal, Red Arrows, na Telecom FC Mechi za CECAFA

Droo ya mashindano ya CECAFA ilifanyika Jumatano 3 Julai 2024, ambapo mabingwa hao wa ligi ya Kenya, Gor Mahia, wamepangwa katika Kundi B wakitarajiwa kumenyana na Al Hilal (Sudan), Red Arrows FC (Zambia), na Djibouti Telkom FC (Djibouti)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *