Gor Mahia Kumenyana na Al Hilal, Red Arrows, na Telecom FC Mechi za CECAFA.

Gor Mahia

Mibabe Wa soka nchini Kenya Gor Mahia watatifuana na Al Hilal wa Sudan, Red Arrows wa Zambia na Telecom FC wa Djibouti, katika  kundi B kwenye michuanao ya CECAFA Kagame Cup mwaka huu. Gor Mahia ambao ni mabingwa wa Ligi kuu ya humu nchini watakuwa wawakilishi wa pekee kutoka Kenya katika michuano hiyo.

Droo ya makundi ilikamilika leo mapema nchini Tanzania, na kundi B linachukuliwa kuwa na ushindani mkali zaidi mwaka huu. Gor Mahia wanatarajia kutumia michuano hii muhimu kama sehemu ya maandalizi kwa ajili ya mashindano ya Klabu Bingwa barani Afrika yatakayoanza mwezi Agosti mwaka huu. Hii itakuwa changamoto ya kwanza kwa kocha mpya wa Gor Mahia, Leonardo Neiva, ambaye anatarajiwa kuimarisha timu na kurejesha hadhi ya kuheshimika katika bara la Afrika.

Mashindano ya mwaka huu ya CECAFA Kagame Cup yatarajiwa kuanza tarehe 9 Julai nchini Tanzania na kuendelea hadi tarehe 21 Julai. Michezo hiyo itapigwa mjini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Azam Complex na Uwanja mpya wa KMC uliopo Kinondoni.

Makundi Kamili ya CECAFA Kagame Cup 2024:

  • Kundi A
    • Coastal Union FC (Tanzania)
    • Al Wadi FC (Sudan)
    • JKU SC (Zanzibar)
    • Dekedaha FC (Somalia)
  • Kundi B
    • Al Hilal (Sudan)
    • Gor Mahia FC (Kenya)
    • Red Arrows FC (Zambia)
    • Djibouti Telkom FC (Djibouti)
  • Kundi C
    • SC Villa (Uganda)
    • APR FC (Rwanda)
    • Singida Black Stars FC (Tanzania)
    • El Merreikh Bentiu (South Sudan)

One thought on “Gor Mahia Kumenyana na Al Hilal, Red Arrows, na Telecom FC Mechi za CECAFA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *