Timu ya taifa ya Kenya inasubiri kwa hamu kuwatambua wapinzani wake kuelekea mechi za kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025, ambazo zitafanyika nchini Morocco. Droo ya makundi ya kufuzu kwa michuano hii itafanyika leo nchini Afrika Kusini mwendo wa saa tisa alasiri.
Harambee Stars, waliokosa kushiriki kwenye makala yaliyopita ya kufuzu kutokana na marufuku ya FIFA, wanatazamia kwa matumaini makubwa kuanza safari yao ya kurejea kwenye mashindano haya. Mara ya mwisho Kenya kushiriki katika kipute cha AFCON ilikuwa mwaka 2019 mjini Cairo, Misri, ambapo walitoka katika hatua ya makundi.
Presenting to you the pots for the #AFCONQ2025 qualifiers. 🤩 pic.twitter.com/mnOy97RBWk
— CAF (@CAF_Online) July 3, 2024
Mechi za kufuzu zitaanza mwezi Septemba mwaka huu, ambapo washiriki wataanza safari ya kuelekea Morocco kwa kipute hicho cha mwezi Desemba 2025. Kenya, iliyoorodheshwa nafasi ya 108 kwenye msimamo wa FIFA, imewekwa kwenye Chungu cha 3 kuelekea droo ya leo.