Kombe la Dunia kwa Wanadada wa U-17 Kung’oa nanga Usiku wa Leo.

Junior Starlets Kombe la Dunia

Michuano ya Kombe la Dunia kwa Wanadada wasiozidi umri wa miaka 17 inatarajiwa kuanza usiku wa leo katika taifa la Dominican Republic, huku mataifa 16 yakijiandaa kupigania taji la mwaka huu. Mashindano hayo yatakayoanza leo, yataendelea kwa muda wa wiki tatu,  na yatamalizika tarehe 3 mwezi Novemba 2024.

Timu ya taifa ya Kenya ya wasichana wasiozidi umri wa miaka 17, maarufu kama Junior Starlets, itapeperusha bendera ya taifa kwenye michuano hii, ikiwa ni mara ya kwanza kwa kikosi chochote kutoka Kenya kushiriki kwenye Kombe la Dunia la Wanadada U-17. Starlets wapo kwenye kundi C pamoja na timu za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Korea, Uingereza, na Mexico.

Kikosi cha Junior Starlets kimekuwa kikiendelea na mazoezi kwa wiki mbili kwenye kambi ya Alicante, Kusini-Mashariki mwa Uhispania, chini ya ukufunzi wa kocha Mildred Cheche. Kenya itaanza kampeni yake kwa kukutana na Uingereza siku ya Ijumaa.

Mashindano haya ni fursa kubwa kwa wanadada wa Kenya kuonyesha uwezo wao kwenye jukwaa la kimataifa, huku nchi nyingine za Afrika zinazoshiriki ikiwa ni Nigeria na Zambia. Nigeria inashiriki kwa mara ya nane, wakati Zambia inashiriki kwa mara ya pili.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *