Olunga, Odada na Anyembe Wako Katika Kikosi cha Stars, Kocha Firat Adhibitisha.

Mkufunzi wa timu ya taifa ya Kenya kwa soka ya wanaume, Harambee Stars, Engin Firat, amethibitisha kwamba wachezaji Michael Olunga, Richard Odada, na Daniel Anyembe watakuwa sehemu ya kikosi kitakachoshiriki katika mechi mbili za kufuzu kwa Kombe la Dunia dhidi ya Burundi na Ivory Coast mwezi ujao nchini Malawi.

Firat alilazimika kutoa ufafanuzi baada ya kikosi kilichotangazwa awali kukosa majina ya wachezaji hao watatu. Katika kikao na waandishi wa habari, Firat alieleza kwamba watatu hao hawatashiriki kambi ya mazoezi ya Stars humu nchini kutokana na majukumu yao katika vilabu vyao, lakini wataungana na kikosi cha taifa nchini Malawi.

Mkufunzi huyo aliweka wazi kwamba nahodha Michael Olunga ni mmoja wa wachezaji wake muhimu zaidi, na hawezi kumwacha nje ya kikosi chake, hasa baada ya kuonyesha umahiri mkubwa katika kipute cha kirafiki cha mataifa manne.

Harambee Stars italazimika kucheza michuano yake miwili ya kufuzu kwa Kombe la Dunia la mwaka 2026 nchini Malawi, kutokana na ukosefu wa uwanja ulioidhinishwa na FIFA kwa mechi za kimataifa humu nchini.

Kikosi cha taifa kilichotajwa na Firat kinawajumuisha wachezaji wafuatao

Walindalango

Patrick Matasi (Kenya Police), Byrne Odhiambo (Bandari), Boniphas Munyasa (Muranga Seal), Ian Otieno (Zesco, Zambia)

Mabeki

Johnstone Omurwa (Estrela, Portugal), Alphonse Omija (Dhofar-Oman).  Amos Nondi (Ararat, Armenia), Brian Okoth (Kenya Police), Abud Omar (Kenya Police), Tobias Knost (SV Verl, Germany)

Viungo

John Ochieng (Zanaco, Zambia), Eric Johanna (UTA, Romania). Adam Wilson (Bradford City, England), Anthony Akumu (Unattached), Kenneth Muguna (Kenya Police), Kaycie Odhiambo (AFC Leopards). Chrispine Erambo (Tusker), Rooney Onyango (Gor Mahia), Ayub Timbe (Sabail, Azeberijan), Duke Abuya (IHEFU, Tanzania), Bruce Kamau (Perth Glory, Australia)

Washambulizi

John Avire (El Sekka El Hadid SC, Egypt), Austine Odhiambo (Gor Mahia), Benson Omala (Gor Mahia), Elvis Rupia (IHEFU, Tanzania)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *