Tamasha la Ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki Lafana Jijini Paris

Olimpiki

Makala ya 33 ya Michezo ya Michezo ya Olimpiki yalifunguliwa rasmi usiku wa kuamkia leo kwa tamasha la kuvutia mjini Paris, Ufaransa. Tofauti na miaka ya zamani ambapo sherehe za ufunguzi zilifanyika kwenye viwanja vya michezo, mwaka huu tamasha hilo lilifanyika kwa mitindo ya kipekee, ambapo wanariadha walipiga gwaride kwenye mto Seine huku wakitumia mashua na meli zaidi ya 80.

Zaidi ya wanamichezo 7,000 walihusika katika gwaride hilo, wakiwa na bendera za mataifa yao, wakizunguka umbali wa kilomita sita katika mto huo wa Seine. Miongoni mwa matukio muhimu, bendera ya Olimpiki ilipandishwa rasmi juu ya mnara maarufu wa Eiffel Tower, ikileta hisia za kipekee kwa wadau wa michezo duniani kote.

Timu ya Kenya iliongozwa na nahodha wa timu ya taifa ya Voliboli, Triza Atuka, pamoja na mshikilizi wa rekodi ya Afrika ya mita 100, Ferdinand Omanyala. Walikuwa sehemu ya gwaride hili muhimu. Olimpiki

Katika makala ya mwaka huu, mataifa zaidi ya 200 yatashiriki na kuonyesha uwezo wao katika fani mbalimbali za michezo. Tunatarajia mashindano haya yatakuwa ya kihistoria na yatatoa burudani ya hali ya juu kwa mashabiki wa michezo duniani kote.

RATIBA YA MASHINDANO YA OLIMPIKI 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *