Tusker Kuvaana na Nzoia Sugar Katika Uwanja wa Dandora Leo

Tusker

Kilabu ya Wanamvinyo wa Tusker itashuka dimbani alasiri ya leo katika mchuano wa ligi kuu ya FKF PL dhidi ya Nzoia Sugar, kwenye mpambano utakaoandaliwa kwenye uwanja wa Dandora.

Tusker, wanaoshikilia nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi, wana imani ya kupunguza pengo la alama kati yao na viongozi wa ligi Gor Mahia. Mkufunzi Robert Matano ameeleza imani yake kuhusu uwezekano wa klabu yake kutwaa ubingwa wa ligi msimu huu, licha ya pengo la alama 14 kati yake na kilele cha jedwali.

Hata hivyo, beki wa Tusker, Daniel Sakari, ametoa onyo kwa wenzake dhidi ya kuwapuuza Nzoia Sugar. Nzoia, ambao wanakabiliwa na hatari ya kushushwa ngazi, wamekuwa katika harakati za kujikwamua na wanatafuta ushindi katika kila mchuano.

Nzoia wanahitaji ushindi katika mechi zao zilizosalia ili kuepuka kushuka daraja kwenda kwenye ligi ya NSL.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *