Wanariadha wa Kenya Watawala Guttenberg Half Marathon

Wanariadha wa Kenya kwa mara nyingine walionyesha uwezo wao wa hali ya juu kwa kutawala na kuibuka kidedea katika mashindano ya Guttenberg Half Marathon yaliyofanyika nchini Ujerumani siku ya Jumapili. Kikosi hicho kilichoongozwa na Benson Mutiso na Victor Kimutai kilichukua udhibiti wa mbio hizo, wakivunja historia ya mbio hizo huku pia wakifanikiwa kumaliza mbio hizo kwa pamoja katika muda wa dakika 61:01. Waandalizi walilazimika kutangaza washindi hao kwa pamoja baada ya kushindwa kuwatofautisha Mutiso na Kimutai.

Mbali na ushindi wa Mutiso na Kimutai, mwanariadha mwingine wa Kenya, Collins Kipkemboi, alimaliza katika nafasi ya tatu kwa muda wa dakika 61:38, akiongeza umaarufu wa Kenya katika mashindano hayo.

Kwa upande wa wanawake, Josephine Naukot na Brenda Jepchirchir wa Kenya waliongoza katika nafasi za kwanza na pili mtawalia, wakimaliza mbio hizo kwa muda wa dakika 69:26 na dakika 69:45. Mbelgiji Hanne Verbruggen alishika nafasi ya tatu kwa muda wake bora zaidi wa binafsi, dakika 70:15.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *