William Muluya Asema K-Sharks Hawatawadharau Sofapaka Wikendi Hii.

Kocha William Muluya

Mkufunzi wa kilabu ya Kariobangi Sharks William Muluya, ameeleza imani kwamba kikosi chake kitatia fora katika mchuano ujao wa ligi kuu dhidi ya Sofapaka wikendi hii.

Muluya ameeleza kwamba anatarajia mtihani mgumu  katika mpambano huo licha ya hali ya kusuasua ya vijana wa batoto ba Mungu kwa sasa hivi. Mkufunzi huyo amesema kwamba hawatawadharau wapinzani wao, na badala yake watawekeza zaidi katika mazoezi yao kabla ya kujaribu uwezo wao wa kuzoa alama zote tatu kwenye mpambano utakaopigwa siku ya Jumamosi katika uwanja wa Dandora mwendo wa saa tisa adhuhuri.

Sharks wamekuwa na matokeo ya kuridhisha katika mechi zao za hivi karibuni, wakifanikiwa kuvuna mabao 15 katika mechi zao tano zilizopita.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *